Job 7:16-19


16 aNinayachukia maisha yangu; nisingetamani kuendelea kuishi.
Niache; siku zangu ni ubatili.


17 b“Mwanadamu ni kitu gani hata umjali kiasi hiki,
kwamba unamtia sana maanani,

18 ckwamba unamwangalia kila asubuhi
na kumjaribu kila wakati?

19 dJe, hutaacha kamwe kunitazama,
au kuniacha japo kwa kitambo kidogo tu?
Copyright information for SwhKC